Header Ads

BASATA waliniharibia sana, najuta kuwataja hadharani wanaume niliotembea nao – Gigy Money

Msanii wa muziki nchini Tanzania, Gigy Money amesema kuwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) lilimuharibia sana kwa kumuita kwa ajili ya mahojiano naye kwani ndio sababu ya watu kujua ujauzito wake.
Akizungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Gigy amesema kuwa alitaka ujauzito wake uwe wa siri lakini alipoitwa na BASATA ilimfanya ashindwe kuficha ujauzito wake.
Nilitaka iwe siri lakini haikuwezekana kipindi kile nilivyoitwa BASATA waliniharibia sana kwani haikuwa siri sana,“amesema Gigy Money.
Tazama tukio la Gigy Money lililomfanya mpaka mimba yake ikaonekana kwa mara ya kwanza.

Kwa upande mwingine, Gigy Money ameeleza jambo analojutia maishani mwake kuwa ni kuwataja wanaume aliowahi kutoka nao kimapenzi katika maisha yake.
Gigy amesema kuwa kitendo cha kuwataja wanaume hao kinamfanya hadi leo baadhi ya wanaume waogope kumtongoza.
Kuwataja wanaume nilipitaga nao najutiaga sana, inafanya kuna muda nikose vitu vya maana kwa kuogopa kuwa nitaropoka. Kumbe ule ni utoto na ni foolish age kila mtu lazima apitie hata uikimbie ni bora uipitie ukubwani usiirudie. Kwahiyo najutia kuwataja wanaume niliowahi kutembea nao ila sijutii kupitia ile hatua,“amesema Gigy Money.
Mwaka jana Gigy Money alitaja wanaume zaidi ya 10 wengi wakiwa mastaa wa muziki wa Bongo Fleva na watangazaji wa Redio na Tv.

No comments:

Powered by Blogger.