Header Ads

RIPOTI: Nigeria yaongoza kwa umasikini duniani

Kama ulikuwa unadhani Somalia ni nchi yenye watu wengi wenye umasikini uliokithiri  basi sahau hilo kwani ripoti mpya ya mwaka 2018 iliyotolewa na Taasisi ya Brookings ya mjini Washington inaonesha Nigeria ndiyo taifa la kwanza duniani lenye
Kupitia tovuti ya Taasisi hiyo, ripoti hiyo imeeleza kuwa Nigeria kwa mwaka 2018 ina watu milioni 87 ambao wanaishi kwenye umasikini uliokithiri ikifuatiwa na India yenye watu milioni 73 huku nafasi ya tatu ikiingia Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.
Ripoti hiyo inaonesha pia nchini Nigeria kila dakika 1 kuna watu 6 wanadumbukia kwenye dimbwi la umasikini uliokithiri wakati huo huo namba ya watu masikini India inazidi kupungua kila kila mwaka.
Hata hivyo, ripoti hiyo pia inakadiria kuwa bara lote la Afrika mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2018 litatengeneza watu milioni 3.2 masikini zaidi.
Kwa upande mwingine ripoti imeeleza kuwa  tangu Mpango wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG’s) uanzishwe mwaka 2016 mpaka mwezi Juni 2018, imeonesha kuwa watu milioni 83 pekee duniani kote ndio wamejikomboa kuuaga umasikini wa kupindukwatu wengi wenye umasikini uliokithiri.

No comments:

Powered by Blogger.