Baada ya Mwigulu Nchemba Kutumbuliwa, Polepole amvaa Zitto Kabwe, Nape Naye Atia Neno
Baada
ya Rais Magufuli kutangaza mabadiliko madogo katika Wizara kadhaa na
aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba kuachwa, Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole na Kiongozi wa ACT
Wazalendo, Zitto Kabwe wameanza kuvutana mitandaoni kuhusu kuachwa kwa
Mwigulu.
Kupitia
mtandao wa wa Twitter Zitto Kabwe amemkaribisha, Dkt. Nchemba kwa
kumwambia sasa ni wakati wake wa kuwatumikia wananchi na kwamba msimamo
wake ndiyo uliomponza.
"Ndugu
yangu Mwigulu Nchemba karibu 'back bench' ufanye kazi ya Wananchi.
Tunajua msimamo wako kuhusu barua ya KKKT umekuponza. Ulikuwa msimamo
madhubuti na ulisimamia haki" - Zitto
Kufuatia
kauli hiyo, Humphrey Polepole katika ukurasa wake, ameamua kumvaa
Kiongozi huyo wa ACT kwa kumuita mzee wa kurukia treni kwa mbele na
kwamba Rais amefanya mabadiliko kutokana na dhamana aliyopewa na Katiba
na si vinginevyo na kumtaka asipotoshe watu.
Polepole ameandika "Mzee
wa kurukia treni kwa mbele ushaanza, mbona unapenda ubashiri na vitendo
vya kilozi? Rais hutenda impendezavyo kwa dhamana aliyopewa Kikatiba".
"Sisi
tuliohudumu kwenye Serikali na Chama tunajua na kuheshimu. Usijitaftize
huruma kwa mtu. Acha kupotosha hiyo si siasa safi. SAD! " Polepole
Kwa
upande wa Mbunge wa Mtama ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Habari, Sanaa,
Michezo na Utamaduni, Nape Nnauye amemkaribisha kiongozi huyo na kumtaka
waungane kuwatumikia wananchi.
"Cde
Karibu Sana! Tuliolelewa humu ni kama Mwanzi, upepo ukivuma Mwanzi
unalala, upepo ukiisha Mwanzi unasimama ukiwa imara zaidi! Tuwatumikie
waliotupa kura!" Nape.
No comments: