Croatia Yaing'oa Denmark Kombe La Dunia Kwa Penalti 3-2 ......Yussuf Poulsen Kuungana Na Ronaldo, Messi Kurejea Nyumbani
Croatia imetinga robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuifunga Denmark anayochezea Yussuf Poulsen kwa penalti 3-2.
Hii
ni baada ya mechi kwisha kwa dakika 120 kukiwa na sare ya bao 1-1, yote
mawili yakiwa yamefungwa ndani ya dakika 4 za mwanzo.
Mikwaju ilikuwa na burudani kubwa huku makipa wa kila upande wakionyesha ujuzi wa kupangua penalti.
Ivan
Raktic ndiye aliyemalizia mkwaju wa mwisho na kuimaliza Denmark ambayo
ilionekana kama ina nafasi ya kusonga baada ya kipa wake, Kasper
Schmeichel kuonyesha ujuzi akipangua penalti mfululizo.
No comments: