BREAKING: Wabunge Wapitisha Bajeti Kuu ya Serikali 2018/ 2019
Wabunge
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameipitisha Bajeti ya Serikali ya
mwaka 2018/19 ya Sh32.45 trilioni kwa kura 266 kati ya 348 sawa na
asilimia 76.
Katibu
wa Bunge, Stephen Kagaigai akitangaza matokeo ya kura leo jioni Juni
26, 2018 amesema jumla ya wabunge waliokuwamo bungeni na kupiga kura
walikuwa 348.
“Idadi
ya wabunge waliopiga kura 348, wabunge 43 hawakuwepo. Kura za hapana 82
na hakuna kura ambayo haikuamua na kura za ndio ni 266,” amesema
Kagaigai
Mara
baada ya kauli hiyo, shangwe kutoka kwa wabunge wa CCM ziliibuka huku
Spika wa Bunge Job Ndugai akiwashukuru Rais John Magufuli, Makamu wa
Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
Amesema
mara baada ya kuondoka Ijumaa, bila shaka mawaziri wataondoka wakiwa
wamesheheni maoni ya wabunge na ushauri ambao kimsingi umetoka kwa
wananchi.
No comments: