Waziri Mkuu Asifu Juhudi Za Aga Khan
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya
Tanzania na Mtandao wa Aga Khan (AKDN ) una lengo la kuleta maendeleo ya
Taifa.
Ameyasema
hayo jana usiku (Jumatatu, Juni 25, 2018) jijini Dodoma wakati
akizungumza na viongozi na wananchi waliohudhuria hafla ya siku ya
IMAMAT pamoja na kuhitimisha maadhimisho ya mtukufu Aga Khan kuwa
kiongozi wa mtandao huo kwa miaka 60.
Waziri
Mkuu alisema maadhimisho hayo yanaonesha kujitolea kwa hali ya juu na
kwa moyo wa dhati ya maisha ya Mtukufu Aga Khan katika kuwahudumia na
kuwalinda watu hususan wanyonge.
"Leo
hii jamii zetu zinanufaika na juhudi hizi za kujitolea kwa hali ya juu
alikokufanya Mtukufu Aga Khan kupitia utoaji wa misaada hasa katika
kuboresha maeneo ya huduma muhimu kama elimu na afya,” alisema.
Alisema
rafiki huyo mkubwa wa Tanzania amechangia kwa kiasi kikubwa kuinua
jamii kiuchumi hususan kwa kupigania kuboreshwa kwa huduma za afya na
elimu kupitia uwekezaji unaofanywa na Mtandao huo wa AKDN.
Waziri
Mkuu aliongeza kuwa maadhimisho hayo yanatoa somo muhimu kuhusu haja ya
kujitolea, na kufanya juhudi za kutosha katika kila jambo sambamba na
kuwahusisha watu wengine.
Hata hivyo, Waziri Mkuu alisema lengo hilo halina budi kuongozwa na nia ya kuboresha maisha ya watu kwa namna yenye staha.
Awali,
Mwakilishi Mkaazi wa Mtandao wa Aga Khan, Bw. Amin Kurji aliipongeza
Serikali kwa kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika maeneo
mbalimbali ya maendeleo.
Alisema
Mtandao wa AKDN umeenea katika mataifa 35 ambako wanatekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo na kwa Tanzania wanatekeleza miradi tisa ikiwemo
ya kilimo, afya, maendeleo ya jamii na elimu.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
No comments: