Kazi Sasa Imeanza: Ureno Kuvaana na Uruguay Huku Hispania Akikipiga na Urusi
Baada
ya mechi nne za jana za kufunga makundi ya A na B kwenye Fainali za
Kombe la Dunia kumalizika, hatimaye mechi mbili za raundi ya 16 bora
zimefahamika ambapo Ureno itacheza na Uruguay huku wenyeji Urusi
wakikabiliana na Hispania
Katika
mechi mbili za Kundi B zilizomalizika jana usiku, zilishuhudiwa
zikimalizika kwa sare ambapo Hispania ilitoka sare ya 2-2 na Morocco
huku Ureno ikitoka sare ya 1-1 na Iran. Hispania itacheza na mshindi wa
pili wa Kundi A ambaye ni mwenyeji Urusi na Ureno itacheza na mshindi wa
kwanza Uruguay.
Katika
mechi ya Ureno dhidi ya Iran zilishuhudiwa penati mbili ambapo
Cristiano Ronaldo alikosa huku Karim Ansarifard akipata kwa upande wa
Iran.
Penati
hizo zimefanya michuano hii kufikisha penati 20 hadi sasa ambayo ni
idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Fainali za Kombe la
Dunia.
Ureno
pia wamefanikiwa kusonga mbele kutoka hatua ya makundi kwa mara ya nne
katika historia yao ya kucheza Kombe la Dunia. Wamefanya hivyo katika
miaka ya 1966, 2006, 2010 na 2018.
Naye
mshambuliaji wa Hispania Iago Aspas ambaye alifunga bao la kusawazisha
la Hispania, sasa amehusika katika mabao 8 kwenye mechi 8 za Hispania
hivi karibuni. Amefunga matano na kusaidia matatu. Hispania pia
wamefanikiwa kumaliza hatua ya makundi bila kupoteza mechi tangu wafanye
hivyo mwaka 2006.
No comments: