Header Ads

Mbunge Hawa Ghasia:Sakata la gesi nilichomewa nyumba yangu moto, nilimpoteza baba lakini kwa hili sitakubali

Mbunge  wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia, amesema yuko tayari kupoteza maisha na mali zake, ili kupigania haki ya wakulima wa korosho kama ilivyokuwa wakati wa kupigania gesi asilia kuwanufaisha watu wa mikoa ya kusini.

Ghasia aliyekuwa waziri wa iliyokuwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), alitoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma jana, alipokuwa anachangia mjadala wa mapendekezo ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka ujao wa fedha na Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2017.

Alisema wakati wananchi wa mikoa ya kusini wakiandamana kupinga kujengwa kwa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, alikuwa serikalini na aliamini usambazaji wa gesi hiyo utanufaisha wananchi wote lakini imekuwa kinyume.
“Kwanza nianze kwa masikitiko makubwa sana ambayo yanasambazwa kwa makusudi dhidi ya Wabunge wanaotetea kupelekewa pembejeo Kwenye maeneo yao.Tuna taarifa jana watu wamekaa vikao waje humu kutudhalilisha Wabunge tunaowatetea wananchi wetu wapate pembejeo.

“Wabunge wote humu ndani tuna haki sawa za kutetea wananchi wetu. Anayetoka Kwenye pamba ataitetea pamba, anayetoka Kwenye madini atatetea madini yake, anayetoka Kwenye korosho ana haki ya kuitetea korosho yake.Mimi napenda niwahakikishie wananchi wanaolima korosho; Wabunge wao tupo imara, tutapambana kuhakikisha haki hii inapatikana. Hata kama haitapatikana, wajibu wetu tutautimiza kama wawakilishi kuja kuwatetea wananchi,” ameongeza

“Mimi nilikaa upande wa serikali wakati wa gesi. Niliitetea Serikali kupeleka gesi kokote Tanzania kwa sababu nilijua serikali inafanya haki. Nilichomewa nyumba yangu moto. Mabomba ya kupeleka maji Kijijini kwetu yaling’olewa. Mikorosho ya Baba yangu ilikatwa. Minazi ya Baba yangu ilikatwa. Katika process hiyo nilipoteza Baba yangu. Bado nilimshukuru Mwenyezi Mungu nilisema Alhamdulilah Alhamdullilah Alhamdulillah! Kwa sababu niliona serikali inachokifanya iko sahihi,” alisisitiza Ghasia.

“Ninachosema kama kuna mtu amefanya ubadhilifu, hata kama ni Hawa Ghasia Kwenye mfuko wa korosho, nipelekeni Mahakamani.Hao wananchi tunaowambia wabunge wa Kusini wabinafsi wanataka kuigawa nchi wana akili na wanajiongeza.”

No comments:

Powered by Blogger.