MADHARA YA KULALA CHALI KWA MAMA MJAMZITO.
Wanawake wajawazito
wanaopenda kulala chali wapo kwenye hatari ya kuzaa mtoto
mfu(stillbirth),kulingana na wanasayansi.
Katika utafiti uliofanyika nchini Ghana, wanawake wajawazito ambao
walipenda kulala chali wakati wa ujauzito walikuwa kwenye hatari mara
tano zaidi ya kuzaa watoto wenye uzito mdogo na kwa wanawake wengine
walizaa watoto wafu.
Utafiti huu ulifanyika nchini Ghana kutokana na kuwa kati ya watoto 1000
wanaozaliwa 20 hadi 50 kati yao huwa ni watoto wafu.Hata hivyo, utafiti
mpya uliofanyika nchini New Zealand pia umehusisha kulala chali kwa
mwanamke mjamzito na idadi kubwa ya watoto wafu wanaozaliwa katika
nchi zenye raia wenye kipato kikubwa.
Mkuu wa utafiti huu,Louise O'Brien kutoka chuo kikuu cha Michigan,
nchini Marekani amesema kama kutokulala chali wakati wa ujauzito
hupunguza uwezekano wa kuzaa mtoto mfu basi ni vizuri kuhamasisha kina
mama wajawazito kutolala chali kwani hii ni njia rahisi na isiyokuwa na
gharama yoyote ile.
Tabia hii ya kulala chali wakati wa ujauzito inaweza kuepukika kwa
kuwashauri kina mama wajawazito madhara yanayopatikana kwa kulala
chali.
Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha ya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya
watoto wanaozaliwa wafu inaweza kuepukika kwa kubadilisha staili ya
kulala tu kwa wanawake wajawazito.
Siku zote madaktari wanashauri kina mama wajawazito kulala ubavu mmoja
hasa upande wa kushoto ili kuepuka kuzaa mtoto mfu au mtoto mwenye uzito
mdogo kwa sababu mwanamke mjazito anapolalia ubavu wake wa kushoto
huongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.
Utafiti huu uliofanyika nchini Ghana unaunga mkono utafiti
uliofanyika hivi karibuni nchini Australia unaojulikana kama Sydney
Stillbirth Study ambao ulisema ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati
wa ujauzito wako kwenye hatari ya mara sita zaidi ya kuzaa watoto
wafu.Utafiti huu wa Australia ulifanyika kwa miaka mitano na ulihusisha
wanawake wajawazito 295 kutoka katika hospitali nane nchini Australia.
Naye mtafiti mkuu katika utafiti huu Dr. Adrienne Gordon, kutoka
Sydney's Royal Prince Alfred Hospital amesema “Tafiti za awali
zilionyesha ya kwamba wanawake wanaolala chali wakati wa ujauzito,
hupunguza mzunguko wa damu unaotakiwa kwenda kwa mtoto.Lakini pia ni
vizuri kwa wanawake ambao ni wajawazito kutotaharuki kama wakati
mwingine watalala chali.’’Kutokana na idadi ndogo ya wanawake wajawazito
waliohusishwa kwenye utafiti huu sisi wana Tanzmed tunachelea kusema ya
kwamba ni vigumu kusema utafiti huu umetoa mapendekezo sahihi ya namna
ya kulala kwa wanawake wajawazito.
Pia kutokana na kutoangalia muda ambao wanawake hao walilala wakiwa
chali (mfano kama walilala masaa 4,6 au 8 kwa siku na kwa siku ngapi) na
tofauti ya hatari kati ya wanawake wajawazito waliolala muda mfupi na
mrefu, hivyo tunawaambia wanawake wajawazito kutohofu kama watalala
chali lakini ni bora kuchukua tahadhari mapema.Tafiti hii inatoa
changamoto kwa watafiti wetu wa afya kuangalia jinsi ya kufanya tafiti
kama hizi katika mazingira ya kwetu.Baadhi ya milalo salama kwa mama
mjamzito
Make Google view image button visible again: https://goo.gl/DYGbub

mjamzito ni kama ifuatayo chini kwenye picha:

No comments: