Mawaziri Wasiopokea Simu Kushughulikiwa
Serikali
imesema iko tayari kupokea malalamiko kutoka kwa Watanzania ambao
wanaona hawakutendewa haki na Mawaziri ikiwemo kutopokelewa simu zao.
Hayo
yameelezwa leo Juni 26 bungeni, na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika.
Mkuchika amesema simu ni sehemu ya mawasiliano.
Mkuchika
ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Jaku Hashim Ayub ambaye
amewashitaki mawaziri akisema kuna mawaziri wamekuwa ni tatizo kwa
kutopokea simu za wabunge hivyo akasema hali inaweza kuwa mbaya kwa
wananchi kama watawapigia.
Katika
swali lake mbunge huyo amesema mawaziri wote wamekuwa ni tatizo kubwa
katika kupokea simu za wabunge wanapowapigia na akataka namba za
mawaziri ziwekwe hadharani kama ilivyo kwa namba za makamanda wa polisi
wa mikoa.
“Hii
ni kwa Mtanzania yeyote akiona hakutendewa haki ikiwemo simu yake
kutokupokewa, aje kutoa taarifa za malalamiko na sisi tutazifanyia kazi
na kama litakuwa gumu kwangu nitapeleka kwa ngazi ya juu,” amesema
Mkuchika.
No comments: