Familia Yakanusha Taarifa za Kifo Cha Mzee Majuto Zinazosambazwa Mitandaoni
Baada
ya kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo
cha Muigizaji Mkongwe nchini, Mzee Amri Majuto, familia yake imeiomba
serikali na vyombo husika ikiwemo mamlaka ya mawasiliano, kuwachukulia
hatua watu wanaozusha taarifa za kifo kwa madai kuwa sasa ni mara ya 10.
Akikanusha
taarifa za kifo cha muigizaji huyo, mtoto wa Mzee Majuto, Hamza Majuto
amesema kuwa kama familia wameziona taarifa hizo kwenye mitandao ya
kijamii na wala hawafahamu nia ya watu hao wanaozusha taarifa za kifo
cha baba yake mara kwa mara.
Aidha
mtoto huyo wa Mzee Majuto amesema kwamba baba yake kwa sasa anaendelea
vizuri tangu aliporudi kutoka nje ya nchi na sasa (Majuto) yupo kwenye
mapumziko kama jinsi ambayo inatakiwa.
"Tangu
jana nimepokea simu na sms zaidi ya 500 zikitaka nithibitishe kuhusu
kifo cha mzee. Kiukweli hii ni mara ya 10 kwa mzee kuzushiwa taarifa ya
kifo. Natambua kwamba kuna vyombo vya usalama pamoja na mamlaka
inayohusika na makosa ya mitandao hivyo hili la kuzusha kifo ni kosa la
jinai naiomba basi TCRA ifuatilie ili kujua dhamira ya huyu mtu ambaye
amekuwa akizusha taarifa za kifo" amesema Hamza.
Hata
hivyo, Kijana huyo amesema kwamba kwa sasa wapo mapumzikoni lakini
hawawezi kusema ni wapi kwa ajili ya kuepusha usumbufu ili kumsaidia
mzee Majuto apate mapumziko mazuri.
No comments: