Header Ads

Nadhani sio rahisi kusaini WCB – Belle 9

Msanii wa Bongo Flava, Belle 9 amefunguka kuhusu kusainMuimbaji huyo ambaye anatamba na ngoma ‘Dada’ ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa anaweza kuwa chini wa usimamizi wa label hiyo ila hadhani kama ni kitu kirahisi.
“Ikitokea tunaweza kusaini lakini kuna condition ambazo nadhani sio rahisi sana kusaini tu moja kwa moja. Inabidi tupate muda kidogo, kuiangalia mikataba ilivyo, kuifikisha kwa wanasheria wangu pia waangalie,” amesema.
“Unajua kwa muda ambao nimekuwepo mimi mwenye najua kabisa nini nahitaji ili kutoka hapa kwenda mbele, kuna jinsi nataka hiyo safari iwe,” amesisitiza Belle 9.
Utakumbuka August 2016 Belle 9 alionekana katika label hiyo akifanya mazoezi na bendi ya Diamond. Hata hivyo muimbaji huyo ameeleza kuwa alifika WCB kwa ajili ya mkataba na Wasafi.com na hakukuwa na zaidi ya hapo.
i katika label ya WCB.

No comments:

Powered by Blogger.