Ufaransa, Argentina, Denmark Na Croatia Zafuzu 16 Bora
Croatia na Argentina zimefuzu kucheza hatua ya mtoano katika 16 za michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi.
Argentina
wamemaliza michezo yao kwenye kundi D wakiwa na alama 4 katika nafasi
ya pili kufuatia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Nigeria jana usiku.
Mabao
ya Argentina yaliwekwa kimiani na Lionel Messi mapema katika dakika ya
14 huku la pili likifungwa na Marcos Rojo mnamo dakika ya 86 ya kipindi
cha pili.
Bao pekee la Nigeria liliwekwa kimiani kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Victor Moses katika dakika ya 51 ya kipindi cha pili.
Wakati
huo Ufaransa pamoja na Denmark zimefuzu kuingia mtoano baada ya sare ya
kutofungana jana mchana katika mchezo wa kundi C.
Kutokana
na matokeo hayo, Ufaransa sasa itakipiga dhidi ya Argentina katika
hatua ya mtoano huku Denmark ikicheza dhidi ya Croatia.
No comments: