Wolper Amwaga Povu Baada Ya Tetesi Za Kutoka na Mr. Nice
Muigizaji
wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amemwaga
povu baada ya tetesi kusambaa anatoka kimapenzi na msanii mkongwe wa
Bongo fleva Mr. Nice.
Siku
chache zilizopita Wolper na Mr. Nice walionekana pamoja wakila bata
Kwenye club moja Nairobi nchini Kenya huku wakionyesha kuwa na ukaribu
fulani.
Kwenye
video ambayo iliwekwa Mtandaoni na Jacqueline Wolper iliwaonyesha
wawili hao wakila bata yaani Wolper akivuta shisha huku Mr. Nice akinywa
pombe ambapo watu mbalimbali walidai huenda wanatoka kimapenzi.
Baada
ya Tetesi hizo za Mahusiano gazeti la Risasi lilimtafuta Wolper kwa
njia ya simu akiwa nchini Kenya na kumuuliza kuhusu ukaribu wake na Nice
ambapo alisema ni wa kawaida tu na wako karibu kwa sababu bosi wao ni
mmoja.
"Watu
wajue sisi tupo kikazi zaidi kwani kuonekana na mtu ni lazima awe
mpenzi wako? Si lazima, huyu ni kaka yangu na bosi wetu ni mmoja,
projekti yetu ikiwa tayari tutaitangaza itajulikana tu lakini kwa sasa
bado ni mapema kuitangaza”.
No comments: