BASATA Wamzuia Diamond Kwenda Kufanya Shoo Nje Ya Nchi
BARAZA
la Sanaa Tanzania (BASATA) limemzuia mwanamuziki, Nassib Abdul
‘Diamond Platnumz’ kwenda kufanya shoo nje ya nchi akiwa katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa sababu
msanii huyo hakuwa na kibali.
Diamond jana alikuwa akielekea katika visiwa vya Madagascar na Mayote ambako atatumbuiza leo (Julai 27) na kesho (Julai 28).
Meneja
wa mwanamuziki huyo, Babu Tale amesema Diamond alitakiwa kuondoka jana
Saa 3.00 asubuhi lakini baada ya kuzuiliwa ilibidi aondoke saa 11.00
jioni baada ya kukamilisha taratibu za kupata kibali hicho.
“Ni
kweli jana msanii wangu (Diamond) alikumbana na mkono wa Basata akiwa
uwanja wa ndege. Kwa kuwa tulishalipwa hela ya watu ikabidi
tukishughulikie kibali haraka ili aweze kuondoka nchini,” anasema.
Hata
hivyo, alilaumu Basata kwa kushindwa kuweka wazi kanuni zake ili
wasanii wazijue badala ya kuwasubiri wakosee ili wawachukulie hatua.
“Ninashauri kama Basata wana chochote wanataka wasanii wakifanye wakishirikishe ili kuepusha mzozo,” anasema.
No comments: