Brazili Yafungasha Virago Kombe la Dunia....Ni Baada ya Kutandikwa 2-1 na Ubelgiji
Kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kimeyaaga mashindano ya Kombe la Dunia kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Ubelgiji.
Walikuwa
ni Ubelgiji walioanza kutikisa nyavu za Brazil mnamo dakika ya 13 tu ya
mchezo kupitia kwa Fernadinho ambaye alijifunga kwa mpira wa kichwa.
Ubelgiji
walikuja tena kambani na kuweka bao la pili kwa mkwaju mkali ulioenda
moja kwa moja nyavuni kupitia kwa Kevn De Bruyne kwenye dakika ya 31
kipindi cha kwanza.
Licha
ya kuamka kwa kasi kipindi cha pili huku wakiutawala mchezo kuliko
Ubegiji, Brazil walikosa nafasi nyingi ambazo kama wangezitumia vema
wangeweza kupindua matokeo.
Mnamo dakika ya 76, Renato Agusto aliweza kuipatia Brazil bao la kufutia machozi na kuufanya ubao wa matokeo kuwa 2-1.
Baada
ya kufunga bao hilo Brazil walionekana kupigana kufa na kupona ili
kusawazisha lakini mpaka dakika 90 zinaisha walikuwa nyuma kwa mabao
hayo mawili kwa moja.
Ubelgiji sasa itacheza na Ufaransa kwenye nusu fainali.
Ubelgiji sasa itacheza na Ufaransa kwenye nusu fainali.
No comments: