Maelfu Ya Vijana Wa Jkt Na Mgambo Wafurika Ofisini Kwa Rc Makonda Kuchangamkia Fursa Ya Ajira
Maelfu
ya Vijana waliohitimu mafunzo ya JKT na Mgambo na hawana kazi jana
walifurika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul
Makonda kwaajili ya kupatiwa ajira ya kusimamia kikamilifu suala la
usafi na kuwatoza faini wanaochafua mazingira.
Akizungumza
na Vijana hao RC Makonda ametangaza Rasmi kutengua kipengele
kilichokuwa kikiwataka Wafanyabiashara kufunga maduka yao siku ya
Jumamosi hadi Saa nne asubuhi kwaajili ya usafi na badala yake
amewakabidhi jukumu hilo vijana wa JKT na Mgambo ambapo watakuwa
wakiwakamata wafanyabiashara watakaokaidi kufanya usafi.
Aidha
RC Makonda amesema vijana hao watakuwa na jukumu la Kusimamia kampuni
zilizopewa kazi ya Usafi kwenye maeneo husika, Kuwakamata, kuwatoza
faini watupaji wa taka pamoja na kufuatilia kujua kila nyumba inapeleka
wapi taka wanazozalisha ambapo ifikapo Jumanne ya Julai 10 itakuwa ndio
mwisho wa usajili wa vijana hao.
Hata
hivyo RC Makonda amewataka vijana hao kutotumia nguvu kuwaadhibi watu
watakaotii Sheria huku akiwahimiza pia kuwakamata vibaka wanaopora Mali
za watu.
Kabla
ya vijana hao hawajaanza kazi watapatiwa mafunzo ya sheria ya mazingira
ili waweze kutekeleza majukumu yao pasipo kumuonea mtu.
No comments: