TCRA yaagizwa kuzishughulikia kampuni za ving’amuzi
Mamlaka
ya mawasiliano nchini (TCRA) imetakiwa kuzichukulia hatua kampuni za
ving'amuzi ambazo zinakiuka leseni kwa kuzuia matangazo ya chaneli za
bure.
Agizo
hilo limetolewa jana Julai 6 na Naibu Waziri wa Mawasiliano na
Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye wakati kamati ya bunge ya
miundombinu ilipotembelea (TCRA).
Mhandisi
Nditiye amesema serikali haitazifumbia macho kampuni zinazoleta michezo
ya kijanja wakati zinafahamu fika maelekezo ya leseni zao.
"Hakuna
kufumbia macho, kama kuna mtu nyumbani kwake hajalipia king'amuzi
halafu amekatiwa chaneli za bure asisite atoe taarifa na hatua
zichukuliwe haraka,"
Amesema
kampuni za Star times, Digitek, Ting na Continental zinatakiwa kurusha
bure chaneli tano za hapa nchini ili kuwapa fursa wananchi kupata
taarifa. Chaneli hizo ni TBC, ITV, Channel ten, EATV na Star TV.
Nditiye
pia ameziagiza kampuni za simu kuzingatia usajili wa laini kwa kutumia
teknolojia ya biometriki ambayo inahusisha uchukuaji wa alama za vidole
na picha ya mtumiaji wa namba husika.
Amesema
mfumo huo wa usajili una lengo la kuhakikisha namba moja ya simu
inatumiwa na mtu mmoja hivyo itasaidia kukabiliana na vitendo vya
matumizi mabaya ya mawasiliano.
"Niwaambie
watanzania kuwa changamoto ya watu kutumia vibaya laini za simu
limeshapatiwa ufumbuzi na linakwenda kumalizika kabisa muda si mrefu
kutokana na mfumo huu,”
“Sasa mtu akisajili namba lazima zichukuliwe alama za vidole na picha apigwe ili tujue kabisa namba fulani inatumiwa na nani,”
Kuhusu utapeli unaofanywa na wanaotuma meseji za kuelekeza fedha itumwe amesema tatizo hilo limeshatatuliwa.
No comments: