Kangi Lugola afunguka tena kuhusu watu wanaopotea Akiwemo Azory Gwanda na Ben Saanane.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amezungumzia tena suala la
baadhi ya watu kutoweka akiwemo mwandishi wa habari wa gazeti la
Mwananchi, Azory Gwanda na msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Ben
Saanane.
Lugola
ameeleza kuwa jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini
uhalisia wa kutoonekana kwa watu hao na kwamba litatoa kauli yake baada
ya kuthibitisha pasipo na shaka kuhusu kilichotokea.
Aliwataka
Watanzania kuachana na uvumi usio na uthibitisho kuwa watu wanaotoweka
wakiwa nyumbani kwao, kama ilivyokuwa kwa Azory wametekwa au kuuawa
kwani Jeshi la Polisi ndilo lenye mamlaka kisheria kuthibisha hilo.
“Sio
kila anayetoweka nyumbani kwake huwa ametekwa au kuuawa kama
inavyovumishwa. Dhana hii inaniumiza na napenda watu waachane nayo,”
anakaririwa na gazeti la Mwananchi.
“Tunaendelea
kuchunguza kubaini sababu za kutoonekana kwao. Hauwezi kusema mtu
amekufa bila kuwa na uthibitisho, na utathibitisha kwa kuuona mwili
wake,” aliongeza.
Wazir
Lugola aliongeza kuwa uchunguzi wa jeshi hilo ni kama jicho ambalo lina
mwisho wa kuona, hivyo utakapofika mwisho wataeleza walichokibaini na
mwisho kufanyia kazi jarada hilo ikiwa ni pamoja na kulifunga.
Ufafanuzi
wa kauli ya Waziri Lugola umekuja ikiwa ni siku chache baada ya kuzua
mijadala alipoeleza kuwa Serikali haiwezi kuingilia uhuru binafsi wa mtu
kutoweka nyumbani kwake na kwenda anapotaka yeye.
Alisema
watu wengi hufanya maamuzi yao wanapoona maisha yanawaendea visivyo, na
huamua kwenda kuishi kokote watakapo na uamuzi wao huo unalindwa na
Katiba ya nchi.
No comments: