Gigy Money Azimikia Umbo la Vanessa Mdee
Msanii wa Bongo fleva Gigy Money amefunguka na kuweka wazi kuwa anavutiwa sana na umbo la msanii mwenzake Vanessa Mdee.
Moja
kati ya vitu ambavyo vilitengeneza headlines kuhusu Gigy Money ni
kupungua ghafla kwa mwili wake na kuzua tetesi kuwa anaumwa na maneno
mengine mengine.
Lakini
Kwenye mahojiano na Clouds Fm, Gigy Money amesema hivi sasa anajithidi
kupunguza mwili wake ili aweze kutumbuiza vizuri jukwaani kama
anavyofanya Vanessa Mdee.
"Kuna
muonekano wa show tofauti na picha za Instagram mimi sasa hivi ni
performer, huwezi kwenda jukwaani una limwili lako tu. Kwa hiyo mtu
unatakiwa na mwili fulani hivi”.
"Do
you look Vanessa akiwa ana-perform, how do you feel unaoana kabisa
machachari, anaweza kuwa na bendi, anaweza kuinua mguu, unafurahi, sio
mtu shabiki anasubiri utikise makalio tu”.
Siku
chache zilizopita Gigy Money alikiri kuwa sababu pekee iliyomfanya
mpaka apungue mwili ni mapenzi ambapo alikuwa anaumizwa na penzi la Baba
watoto wake Mo J.
No comments: