Idris Sultan Atangaza Ujio Wa Kipindi Chake Azam TV
Mchekeshaji
na Muigizaji wa Bongo movie Idris Sultan ametoa habari njema kwa
mashabiki zake baada ya kutangaza ujio wa kipindi chake kwenye Tv yako.
Idris
alitangaza Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa kipindi chake
kilichokuwa kinaruka Kwenye ukurasa wake wa YouTube Kitaanza kuonekana
rasmi ndani ya Wasafi Tv.
"Nakumbuka
wakati SIO HABARI ni show ndogo tu. Nilipoanza lengo kuu ilikuwa
kujaribu kusema mambo makubwa na mazito ambayo wengi wanayajua,
wanayasikia na labda hawataki kuyaongelea au wanaogopa. Haya mazito
tuliyadadavua katika lugha nyepesi na ya kufurahisha na ujumbe ulifika.
"Show
ilikaa mwezi tu kwenye TV nikaikatisha kwasababu niligundua ni kubwa
kuliko nilivyoichora na ilibidi nifanye hivyo ili isianguke. Ilikua ni
show nimelenga vijana tu ila kila jumatatu zilikaa familia kuangalia SIO
HABARI.
"Wakubwa
kwa wadogo. Haya niliyajua kwenye malalamiko baadhi ya watu wakisema
samahani Idris punguza makali ya maneno tunaangalia na wazazi wetu
“mnaogopa wazazi wataharibika au ?”
"Nilisema
ila nikagundua nini kimesemwa bila wao kujua.This is not just a show
anymore, hii ni sauti ya wengi wasioweza, ni kitu kimoja chenye ukweli
mwingi kinachounganisha familia nzima na kumsikiliza mpuuzi mmoja
anayetoa la moyoni.
No comments: