Nay Wa Mitego Adaiwa Kuvunja Mahusiano na Nini Baada Ya Familia Yake Kutaka Ndoa
Msanii
wa Muziki wa Bongo fleva Nay Wa Mitego amedaiwa kuvunja Mahusiano na
mpenzi wake Nini baada ya familia ya Nini kutaka afunge ndoa na binti
yao.
Shilawadu
wanaripoti kuwa Nay wa Mitego na mpenzi wake Nini wamejikuta katika
wakati mgumu baada ya familia ya Nini kumkalia kooni Nay na kumtaka
amuoe Nini.
Nay
na Nini wamekuwa Kwenye Mahusiano kwa muda kidogo Lakini sasa inadaiwa
Familia ya Nini imekuja juu na kumtaka Nay amuoe binti yao baada ya
kukaa naye nyumbani kwake.
Inadaiwa
Nini alihamisha makazi yake nyumbani kwa Nay na kila Familia yake
ilikuwa ikimtafuta arudi nyumbani alikuwa anagoma ndipo walipoamua
kumsaka na kumtaka afunge ndoa.
Lakini inasemekana kuwa Nay alikuwa anawapiga chenga kila wakimtafuta anajificha hataki kabisa kuonana na Familia ya Nini.
Siku
ya leo Nay wa Mitego Kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza
kumtosa Nini na kudai yupo single ambapo kupitia ukurasa wake wa
Instagram alisema “It’s Official I am Single”.
No comments: