Picha: Japan yaacha ujumbe wa shukrani ‘dressing room’ na kufanya usafi uwanja mzima
Licha ya kupokea kipigo cha jumla ya mabao 3 – 2 dhidi ya Ubelgiji na
kuyaaga mashindano Japan imeonyesha mfano huo wa kuigwa na mataifa
yaliyoshiriki baada ya kuhakikisha wamesafisha chumba chao cha
kubadilishia nguo huku maelfu ya mashabiki wakifanya usafi kwenye uwanja
waliyochezea hapo jana jambo ambalo ni nadra kufanywa na timu shiriki.
Wachezaji wengi wa Japan walionekana wakibubujikwa na machozi baada ya kutolewa kwenye mashindano hayo kwa bao la mwisho la Nacer Chadli na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 3 – 2 dhidi ya Ubelgiji.
Taarifa kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani FIFA kupitia ukurasa wake wa Twitter umeandika kuwa kikosi cha Japan kimeacha ujumbe wa shukrani kwa waandaji wa mashindano hayo Urusi.

No comments: