ACT Wazalendo Yawataka Nape, Bashe na Hawa Ghasia Wahame CCM, Wajiunge ACT- Wazalendo
Katibu
wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ACT Wazalendo, Ado Shaibu amefunguka
kuwa hakuna mwanaharakati anayeweza kulitetea Taifa akiwa chini ya Chama
tawala.
Shaibu
amefunguka hayo katika mkutano wa wake na wanahabari jan, katika ofisi
za Chama hicho ambapo alisema kuwa endapo wabunge, Nape, Bashe na Hawa
Ghasia wana nia ya dhati ya kuwatetea wanyonge wahamie ACT-Wazalendo.
“Wabunge
wanaotetea haki za wanyonge, wakina Nape, Bashe na Hawa Ghasia
haiwezekani kufanya harakati za kuwatetea wanyonge huku mkiwa CCM, sana
sana mtaonekana waasi katika chama chenu njooni kwetu”, alisema Shaibu.
Hayo
yamejiri ikiwa ni siku chache kabla ya kuahirishwa kwa vikao vya Bunge,
liliibuka sakata la korosho lililokuwa likiendelea katika vikao vya
Bunge, ambapo Wabunge wa CCM ambao waliokuwa wakilipigia kelele suala
hilo ni Hussein Bashe, Nape Nnauye pamoja na Hawa Ghasia.
No comments: