Apandishwa kizimbani kwa kumkashifu Rais Magufuli kwa Maneno “Rais kitu gani bwana”.
Mkazi
wa Wilaya ya Ngara, Kagera Justin Emmanuel (31) amefikishwa Mahakama
ya Wilaya Misungwi mkoani Mwanza, kwa tuhuma ya kutoa lugha chafu dhidi
ya Rais John Magufuli.
Mwendesha
mashtaka wa polisi Ramsoney Sarehe alisoma hati ya mashtaka mbele ya ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Erick Marley leo Julai 3.
Sarehe amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria namba 89 (1) ya mwaka 2002.
Amesema mshtakiwa alitoa lugha ya kumdhihaki Rais Juni 25 katika Kivuko cha Kigongo saa 10:00 jioni kwa kutamka maneno ya “Rais kitu gani bwana”.
Hata hivyo mshtakiwa alikana kosa hilo na hakimu aliahirisha shauri hilo hadi Julai 26 itakapotajwa tena mahakamani.
Mshtakiwa
yupo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya kuwa na mdhamini
mmoja aliyewasilisha bondi ya mali isiyohamishika yenye thamani ya
Sh500, 000.
No comments: