Serikali Yatengua Katazo la Wananchi Kuzuiwa Kupanda Meli
Naibu
Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Atashasta Nditiye ametengua katazo la
wananchi kuzuiwa kupanda meli ya serikali hadi wawe na vitambulisho vya
uraia au cha mpiga kura jijini Mwanza.
Nditiye
amesema kuwa utaratibu wa awali uendelee kutumika hadi pale watakapo
kaa upya kujadili ni njia ipi sahihi itakayoweza kuwawezesha wananchi
kupata huduma ya usafiri bila kikwazo.
Nditiye
ameongeza kuwa suala hilo lilitokana na kutokuwa na maelewano mazuri
baina ya Shirika la Meli pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama jijini
humo.
“Wananchi
wanamatatizo mengi, unapoanza kumchanganya na mambo ya vitambulisho
tena unakuwa unawavuruga naomba utaratibu wa awali utumike na tuangalie
utaratibu mwingine hapo baadaye”, amesema Nditiye.
Mamia
ya abiria waliotakiwa kusafiri kwa meli ya Mv.Nyehunge kutoka jijini
Mwanza kuelekea wilayani Ukerewe wamekwama kwa siku nne katika bandari
ya Mwaloni Kirumba jijini humo baada ya kushindwa kutekeleza sharti
linalomtaka kila msafiri kuwa na kitambulisho rasmi cha uraia au kupigia
kura.
No comments: