Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Kamuagiza RPC kuwachukulia hatua mkuu wa kituo Kwa Rushwa
Mwenyekiti
wa Kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira
amemtaka Kamanda wa Polisi mkoani humo kumchukulia hatua za kinidhamu
Mkuu wa Kituo cha Polisi Mwanga na askari wa kituo kidogo cha polisi
Nyumba ya Mungu na Lang'ata wilayani kutokana na tuhuma za rushwa dhidi
yao.
Mghwira
ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,ametoa agizo hilo jana Julai
21,wakati akizungumza kwenye mkutano wa Hadhara katika Kata ya
Lang'ata,Wilaya ya Mwanga.
Katika
Mkutano huo ambao, uliohudhuriwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM, Humphrey Polepole, na viongozi wengine wa chama na
serikali,Mghwira alisema Askari hao wamekiuka taratibu na kujiingiza
kwenye vitendo vya rushwa,hatua ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika
jitihada za kudhibiti uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu.
Alisema
Askari hao wamejianzishia vituo vyao vya ushuru na kuanza kukusanya
mapato yatokanayo na uvuvi haramu katika Bwawa la Nyumba ya Mungu,ambalo
lilifungwa baada ya kukithiri kwa uvuvi haramu na samaki kupotea.
"Naomba
niseme Askari wa Lang'ata na Nyumba ya Mungu mmenikwaza,kwani kituo
chenu kipo juu na mtu hata awe mfupi kunizidi anaweza kuona mazingira
yote ya Bwawa na kuona wavuvi haramu,lakini wao huwa hawawaoni, hii ni
hatari sana,naomba RPC uwaondoe mara moja na kuwachukulia hatua,"alisema
Mghwira.
Mkuu
huyo ambaye alitangaza kulifunga Bwawa la Nyumba ya Mungu kwa
Muda,alisema serikali ilikuwa na nia njema kulifunga Bwawa hilo,lakini
Askari wamepoteza malengo ya serikali na kukwamisha mpango wa kuacha
samaki wawe wakubwa.
Akizungumza
katika kikao hicho, Polepole alisema serikali haitawavumilia askari au
watendaji watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa na kuchafua
utendaji mzuri wa Serikali ya awamu ya Tano.

No comments: