Waziri wa Afya: “TFDA isiwe chanzo cha vikwazo katika juhudi za Tanzania ya Viwanda"
Mamlaka
ya chakula na dawa TFDA imetakiwa kuwa chachu ya uchumi wa viwanda
hususani katika kuzalisha dawa hapa nchini ili kupata matokeo chanya
katika hatua ya kuinua uchumi wa viwanda.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kukabidhi vyeti vya ithibaki kwa kiwango cha kimataifa ISO 17025 kwa maabara ya chakula na maikrobailojia za TFDA.
“TFDA
isiwe kikwazo kwa wawekezaji nchini hususan Viwanda vya kuzalisha dawa
ili kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.John Magufuli ya kuelekea uchumi wa viwanda”
Aidha,Waziri
Ummy amesema TFDA wanawajibu wa kuwawezesha wafanyabiashara kutoa
bidhaa zao wanazozileta nchini mapema zaidi Mara wanapokuwa
wamejiridhisha na ubora unaokidhi afya za watanzania na kuwapa vibali
mapema.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA
)Agnes’s kijo amesema wanawajibu wa kuimarisha afya za watanzania na
kuimarisha maabara zao kwa viwango vinavyokubalika kitaifa.
Kijo
amesema vyeti hivyo vya kimataifa ni ishara kubwa inayoonyesha Kuwa
TFDA inafanya kazi katika kudhibiti ubora wa bidhaa hususan vyakula na
dawa ili kujenga afya za wananchi.
TFDA
imepokea vyeti vya uthibiti kwa kiwango cha kimataifa kwa maabara ya
chakula na daea ambapo wamefanya vizuri katika upimaji wa vyakula na
dawa vinavyoingia na kutoka nchini.
No comments: