Casto Dickson Ataja Sababu Za Kuchora Tattoo Ya Tunda
Mtangazaji
wa kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds Tv, Casto Dickson amefunguka na
kutaja sababu zilizomsukuma mpaka kufikia uamuzi wa kuchora tattoo ya
jina la Tunda mkononi mwake.
Siku
ya jana Casto alianika tattoo yake mpya Kwenye ukurasa wake wa
Instagram na kuonyesha jinsi gani amekolea kwa mpenzi wake huyo mpaka
kuamua kuchora Jina lake.
Casto amesema kuwa alitumia dakika 10 kuamua achore tatoo hiyo na hawezi juta kwa kuwa ameutendea haki moyo wake.
"Mimi
nimechora ile tattoo kwa sababu kiukweli nampenda yule mwanamke na siko
naye kwa ajili ya kumpitia, Hapana ila tuna malengo na kila mtu
amepanga atabadilika na tumeamua kufanya maisha.
"Tunda
ndio mwanamke pekee ambaye nimechora jina lake mwilini mwangu kwahiyo
watu watambue kuwa ana maana sana kwangu halafu kuna wanaosema kuwa ni
mapema sana kwa mimi kuchora Tattoo ....ninachotaka watu wajue ni kuwa
tumekuwa pamoja kwa muda, mrefu mapenzi yetu hayajaanza jana wala juzi”.
Lakini
pia Casto amesisitiza kuwa hata kama wakiachana yeye na Tunda hawezi
kufuta ile tattoo lakini amesema anajua kuwa hawawezi kuachana, watakuwa
wote milele.
No comments: