Meneja wa Diamond Aitibua Mahakama.
Meneja
wa msanii Diamond Platnumz anaejulikana kama Babu Tale ameitibua
mahakama baada ya kutakiwa kufika mahakamani jana lakini hakufika
kufika kwa madai ya kuwa nje ya nchi huku akiwa alishakatazwa kutoka
nje ya nchi ikiwa kesi yake ikiendelea mahakamani.
==
Meneja
huyo anakabiliwa na kesi ya madai baada ya kampuni yake kufanya
matangazo na baishara ya kanda za dini za shekhe mmoja jijini Dar es
salam bila ridhaa yake na kuamuliwa kulipa fidia lakini alishindwa
kulipa fidia hiyo.
Babu Tale alitakiwa kufika mahakamani jana kusikiliza uamuzi wa shauri lake kuhusiana na uhalali wa amri ya mahakama hiyo kumkamata na kumfunga jela kama mfungwa wa madai baada ya kushindwa kulipa fidia.
Hata hivyo hakutokea, badala yake alifika kaka yake Idd Shaban Taletale. Wakili wao, Issa Chondo aliieleza mahakama kuwa Babu Tale hayupo mahakamani kwa kuwa amesafiri nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.
Kitendo cha kusafiri nje ya nchi bila kutoa taarifa na hivyo kushindwa kufika mahakamani kilimfanya Jaji Mkasimongwa aseme kuwa alichokifanya Babu Tale si cha kiungwana, kauli aliyoirudia mara tatu kuonyesha kuwa kilimuudhi.
Awali Wakili Chondo alidai kuwa mteja wake amekwenda kutibiwa nchini Afrika Kusini, lakini alipobanwa maswali na jaji alijikuta akibadili kauli yake na kusema hajui amekwenda nchi gani, huku akiiomba Mahakama imruhusu awasiliane naye kumuuliza.
Maelezo ya wakili huyo yalimshangaza jaji na kumhoji wakili huyo kuwa inawezekanaje mteja wake ambaye yuko kwenye amri ya kukamatwa asafiri nje ya nchi bila kumuaga wakati anajua kuwa anatakiwa mahakamani.
“Lakini si anajua yuko under arrest? (chini ya amri ya kukamatwa?) Inawezekanaje amekwenda nje ya nchi bila taarifa, sasa huu si uchokozi?” alihoji Jaji Mkasimongwa baada ya Wakili Chondo kutoa taarifa kuwa mteja wake amesafiri nje.

No comments: