Waziri Mkuu Kuzindua Vituo 51 Vya Hali Ya Hewa Vinavyo Jiendesha Vyenyewe,
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa
anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Vituo 51 vya Hali ya Hewa
vinavyojiendesha vyenyewe, Vituo 15 vya Kupima wingi wa maji Mtoni,
Kanzidata ya Taarifa za Hali ya Hewa pamoja na Kituo cha Operesheni na
Mawasilino ya Dharura.
Uzinduzi
huo utafanyika Jumatano, tarehe 27 Juni, 2018 katika Makao Makuu ya
Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma. Shirika la Utangazaji la
Taifa (TBC1) litaonesha shughuli hiyo mubashara kuanzia saa sita mchana.
Akizungumza
wakati wa maandalizi ya Uzinduzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama pamoja na kuwakaribisha wananchi wote kushiriki katika
uzinduzi huo, amebainisha kuwa Kuzinduliwa kwa vituo hivyo , kanzidata
na kituo cha Operesheni na Mawasiliano nchini ni baadhi ya jitihada
zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano kwa kushirikiana na wadau wa
maendeleo katika kuhakikisha menejimenti ya maafa inaimarika nchini.
“Vituo
hivyo vitawasaidia Watanzania ambao ni wadau wakubwa wanaotumia Taarifa
za Hali ya Hewa katika kupata taarifa za awali za utabiri wa uwepo wa
majanga au kutokuwepo ili kujiandaa, kuyakabili endapo majanga yatatokea
pamoja na kusaidia katika maandalizi ya shughuli za maendeleao ikiwemo
upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kusaidia kupanga aina za mazao
yanayofaa kulimwa kulingana na mabadiliko ya tabia nchi”, amesema
Mhagama
Ofisi
ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa Kuimarisha Taarifa za Mabadiliko ya
Tabianchi na Uboreshaji wa Mifumo ya Tahadhari za Awali, imeweza
kuimarisha miundombinu na mazingira ya kufuatilia taarifa za mabadiliko
ya tabianchi na kutengeneza mifumo imara ya kutoa tahadhari za awali,
usimamizi wa maafa na kuchangia katika mipango ya maendeleo endelevu.
Mradi
wa Kuimarisha Taarifa za Mabadiliko ya Tabianchi na Uboreshaji wa
Mifumo ya Tahadhari za Awali, Uliandaliwa kwa pamoja kati ya Serikali
ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na
kufadhiliwa kupitia Mfuko wa Uboreshaji wa Mazingira Duniani (GEF).
Mradi umetekelezwa na Wizara na Taasisi za Serikali ikiwa ni pamoja na
Ofisi ya Makamu wa Rais, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Wizara ya Kilimo
na Mamlaka ya Hali ya Hali ya Hewa Tanzania, tangu mwaka 2014 hadi
Juni mwaka 2018.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILINO SERIKALINI
OFISI YA WAZIRI MKUU
No comments: