Mume na Mke Wateketea kwa Moto.....Ni Baada ya Mwanaume Kufunga Mlango na Kisha Kuwasha Moto
Mume
na mke, wamefariki dunia leo Juni 26 baada ya mwanaume huyo, kufunga
mlango wa nyumba kwa ndani, kisha kutia moto nyumba hiyo.
Imeelezwa kuwa, tukio hilo limetokea, usiku wa saa saba, mnano Juni 25 katika eneo la Kilimahewa, Mailimoja, Kibaha.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa, chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Pwani Jonathan Shanna amemtaja mwanaume huyo kuwa ni
Hussein Zaid (58) na mwanamke ambaye amefariki katika tukio hilo ni mke
wake mdogo, Zainabu Juma (42).
“Siku
ya tukio hilo Hussein alijaribu kujiua akiwa amejifungia ndani ya
nyumba yake pamoja na mkewe huyo kwa kuzikusanya nguo zilizokuwa humo na
kuziwasha moto kwa kutumia kiberiti,” alisema Kamanda Shanna na
kuongeza:
"Kabla
ya kutekeleza tukio hilo kwanza alijaribu kumchoma mke wake huyo kwa
kisu na alipoona hajafanikiwa ndipo alipoamua kuichoma moto nyumba wote
wawili wakiwa ndani.”
Ameongeza kuwa baadhi ya majirani walifika kutoa msaada na kuwajulisha Polisi ambao walifika eneo hilo.
“Hata
hivyo, licha ya kuwaokoa wote wawili wakiwa hai, kisha kuwapeleka
Hospitali ya Tumbi, lakini walihamishwa Hospitali ya Muhimbili ambako
walifariki dunia wakipata matibabu hospitali,” alisema
No comments: