Mwanasheria Mkuu wa Serikali Awajibu Wabunge Waliotaka Ahojiwe na Kamati ya Maadili kwa Kulipotosha Bunge
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali (AG), Dk Adelardus Kilangi amewajibu wabunge waliotaka
ahojiwe na Kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa madai ya
kukidanganya chombo hicho cha Dola kuwa fedha za ushuru wa mauzo ya
korosho nje ni za umma.
Wabunge
waliomuomba Spika Job Ndugai kuitaka kamati hiyo kumhoji na kumchukulia
hatua AG ni Zitto Kabwe (Kigoma Mjini) na Cecil Mwambe (Ndanda).
Akiwajibu
wabunge hao AG amesema si kweli kuwa ushuru huo ulianzishwa na Serikali
si wakulima, kwamba Bodi ya Korosho ilikuwa ikikusanya kwa niaba ya
Serikali.
“Tozo
hii haikuanzishwa na wakulima. Bodi ya korosho ilianzishwa kwa sheria
ya mwaka 1984 . Lakini mwaka 1998 kulitokea ubadhilifu fedha, Serikali
ilitoa maelezo kuwa fedha zisipelekwe mfuko wa Korosho,”amesema.
Amesema
mfuko huo haukuridhika na maelekezo ya Serikali na hivyo ikafungua kesi
Mahakama Kuu na kutoa uamuzi kuwa bodi ya korosho inakusanya fedha za
Serikali na Serikali ina mamlaka na fedha hizo.
“Mfuko
haukuridhika, ukakata rufaa lakini mahakama ya rufaa ilitupilia mbali
rufaa hiyo hivyo kisheria uamuzi wa mahakama kuu unabaki ule ule (kwamba
fedha hizo ni za umma),”amesema kilangi.
Kuhusu
kauli ya kwamba wakulima wa korosho waliingia mkataba na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) ya kukusanya kodi, mwanasheria huyo amesema hakuna
mtu anayeweza kupatana na TRA kukusanya kodi.
“Hatuna
mtu yoyote anaweza kukusanyiwa kodi na TRA. Huu ni upotoshaji.
Marekebisho ya Sheria ya Korosho ya mwaka 2009 hayatambui mfuko wa
kuendeleza korosho. Haiwezekani kuutambua mfuko kisheria,”amesema.
Amesema
kwa mujibu wa Katiba na sheria za fedha, TRA ikishakusanya fedha
inatakiwa kupeleka katika mfuko mkuu wa Serikali, hivyo kufanya vingine
ni kuvunja Katiba na Sheria.
Kuhusu
kufuta Tume ya Mpango, Dk Kilangi amesema kufuta tume hiyo hakuna shida
kwasababu majukumu yake yatahamishiwa kwenye wizara na kwamba sheria
inaweza kutungwa upya kwasababu hakuna shida katika hilo.
No comments: