TRC yahamasisha wafanyabiashara wanaokwenda Uganda kutumia reli
Shirika
la Reli Tanzania (TRC) limewataka wafanyabiashara wanaosafirisha mizigo
kwenda Uganda kutumia njia ya reli kwa kuwa ni salama na nafuu.
Kaimu
Naibu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa TRC Focus Makoye amewahakikishia
wafanyabiashara kuwa shirika hilo limejipanga vilivyo kutoa huduma hiyo
ambayo ilisitishwa miaka 10 iliyopita.
Makoye
ameyasema hayo jana jioni ya Juni 28 ikiwa ni muda mfupi kabla ya
kuanza kusafirisha mzigo wa tani 2400 za mafuta mali ya Shirika la
Mpango wa Chakula Duniani (WFP) unaopelekwa nchini Uganda.
Amesema kuanza kwa safari hizo ni hatua mojawapo ya kulifufua shirika hilo hivyo wafanyabiashara wachangamkie fursa hiyo.
"Ni furaha kubwa sana kwetu tumeanza safari hii tukiwa tumejipanga kabisa na tunawahakikishia wafanyabiashara kuwa tuko vizuri,
"Wote
tunafahamu usafiri wa reli ndio wa gharama nafuu na uhakika, hivyo basi
tunawakaribisha watu wengi zaidi ambao wanafanya biashara kati ya
Tanzania na Uganda watumie usafiri huu,"amesema
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha lojistiki cha WFP Mahamud Mabuyu
amesema wamevutiwa kutumia njia ya reli baada ya kuhakikishiwa usalama
wa mzigo.
Kwa
mujibu wa Mabuyu usafirishaji kwa njia hiyo pia unasaidia kuokoa dola
40 kwa kila tani ambayo ingesafirishwa kwa kutumia magari.
"Mwaka jana tulishasafirisha tani 16000 kwenda Dodoma na Isaka, mzigo wetu ulifika salama haikupotea hata mfuko mmoja,"
"Hilo
limetuvutia na baada ya hizi tani 2400 kuondoka ndani ya muda mfupi
tutapeleka tena tani 15,000 hiyo ni kudhihirisha ni kiasi gani
tunaridhishwa na TRC,” amesema
No comments: