Rais Magufuli kufanya ziara ya kihistoria nchini Kenya
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
anatarajiwa kuzuru nchini Kenya mwezi ujao katika ziara ambayo itakuwa
ya kihistoria.
Rais
Magufuli kwenye ziara yake ataungana na Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi
wa upinzani nchini humo Raila Odinga na kisha kutembelea katika Kaunti
ya Nyanza.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la Nation la nchini Kenya
limeeleza kuwa Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili nchini Kenya Ijumaa ya
wiki lijalo.
Gazeti
hilo pia halijaeleza ziara hiyo itakuwa ya siku ngapi na itakuwa na
lengo gani katika kipindi hiki ambacho Rais Uhuru Kenyatta na Odinga
wameonekana kupatana na kuweka tofauti zao za kisiasa kando.
Hii ni mara ya pili kwa Rais Magufuli kuzuru nchini Kenya ni baada ya kuzuru mwaka jana ambapo alikutana na Rais Uhuru Kenyatta.
Hata
hivyo, Rais Magufuli hata kabla ya kukutana na Kenyatta mwaka 2016
kwenye ziara yake nchini Kenya mwaka huo huo alitembelewa na Raila
Odinga kijijini kwake Chato..
Ziara
hiyo inakuwa ni ya kihistoria na ya kwanza kwa Rais Magufuli kukutana
na viongozi hao wawili na wenye nguvu zaidi kwenye siasa za Kenya.
No comments: