Rais Magufuli afurahishwa na Tuzo ya Grace
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,
amefurahishwa na ushindi alioupta mjasiriamali Dr. Elizabeth Kilili
ambaye amepata tuzo nchini Marekani kupitia bidhaa zake za 'Grace
product'.
Rais
Magufuli ameeleza furaha yake hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa
Twitter ambapo zaidi amesifu namna ambavyo Dr. Elizabeth alitumia fursa
hiyo kukitangaza Kiswahili baada ya kukitumia wakati akishukuru umati wa
watu waliokuwepo ukumbini.
Sherehe
za utoaji tuzo hizo maarufu kama 'International Quality summit' kwa
mwaka 2018 zilifanyika May 27-28 2018, jijini New York nchini Marekani.
Tuzo hizo ambazo hutolewa kwa makundi maalum ikiwemo viongozi pamoja na
wazalishaji wa bidhaa asili zimefanyika kwa mara ya 32.
''Nimefurahishwa
na ushindi wa Grace Products, lakini pia nimefurahishwa kwa kutumia
Kiswahili kukizungumza nchini Marekani, hongereni sana Grace Products''.
ameandika Rais.
No comments: