Waziri Mpango Asema Ataitembelea Mikoa ya Kusini....Hakuna Wa Kumzuia na Yupo Tayari Hata Kufa
Waziri
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema atatembelea mikoa ya
Lindi na Mtwara licha ya vitisho vilivyopo na yuko tayari kufa, na kamwe
hawezi kuihujumu mikoa hiyo kiuchumi na hakuna anayeweza kumzuia
kuitembelea katika kutekeleza majukumu yake.
Dkt.
Mpango ametoa kauli hiyo leo, Bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha
hoja yake ya Bajeti ya Serikali aliyoiwasilisha Juni 14 mwaka huu,
ambapo amesisitiza kuwa hakuna mtu wa kumzuia na iwapo kuna mwenye chuki
binafsi anamwombea msamaha kwa Mungu..
“Kama
yupo mtu ana chuki binafsi na Philip Mpango namwombea msahama kwa
Mwenyezi Mungu, na niwatahadharishe wanaokula fedha za umma wanakula
sumu,” amesema Dkt. Mpango.
Waziri
Mpango Ameongeza, “Mimi Philip Mpango siwezi kamwe kuwahujumu wakulima
wa mkoa wa Lindi na niwahakikishe watanzania kuwa Mtwara na Lindi
nitakwenda iwe kutimiza wajibu wangu na ni uhuru wangu na hata ikibidi
kufa katika kulitumia taifa” ameongeza Waziri Mpango.
Amesema
amewatumikia Watanzania wote bila ubaguzi, amefundisha wanafunzi wote
wakiwamo wanaotoka mikoa ya Kusini bila upendeleo na amewahi kuwa
mshauri wa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete na hakuwahi kuwa na
upendeleo.
Tayari
baadhi ya wabunge wametishia kufanya maandamano iwapo Serikali haitatoa
asilimia 65 za ushuru wa mauzo ya korosho nje kwa ajili ya maendeleo ya
zao hilo, huku wakipinga mabadiliko ya Sheria ya Korosho yanayokusudiwa
kufanywa na Serikali ili ushuru huo upelekwe katika Mfuko Mkuu wa
Hazina.
No comments: