Spika Ndugai: Wabunge Mkiikataa Bajieti Hii Rais Atalivunja Bunge
Spika
wa Bunge Job Ndugai amesema kama wabunge wataipigia kura ya hapana
Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19, Rais atalivunja Bunge.
Spika
Ndugai ametoa kauli hiyo leo asubuhi bungeni Juni 26, 2018 wakati
akitoa maelezo ya kile kitakachofanyika leo saa 11 jioni ya kuipitisha
bajeti.
“Endapo mlio wengi mtaikataa Bajeti ya Serikali, Bunge hili Rais atalivunja haraka,” amesema Spika Ndugai.
Baada ya kauli hiyo, minong’ono ya kutoka pande zote za wabunge ilisikika. Spika Ndugai hakuishi hapo, akasema tena:
“Na baadhi yenu, mkirudishwa majimboni hamrudi kwa hiyo akili za kuambiwa changanya na zako.”
Amewaomba
wabunge wote kuwapo bungeni ifikapo saa 11 jioni huku akisisitiza
kwamba mbunge hapigi kura kwa jambo moja, bali ni kwa mfuko wote wa
bajeti, kwa hiyo ni vizuri wananchi wakaelewa.
Katika
hatua nyingine, Spika Ndugai amesema kuanzia sasa bendi ya muziki ya
polisi, (Brass Band) itaingia bungeni kuongoza wimbo wa Taifa kabla na
baada ya kikao cha Bunge kuanza.
No comments: