Bunge laomboleza Kifo cha Mbunge Profesa Maji Marefu
Spika
wa Bunge Job Ndugai ameeleza kusikitishwa na kifo cha Mbunge wa Korogwe
Vijijini, Stephen Ngonyani aliyefariki usiku wa kuamkia leo wakati
akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
jijini Dar es Salaam.
“Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa
Jimbo la Korogwe Vijijini mkoani Tanga, Mheshimiwa Stephen Ngonyani,
maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu, kilichotokea usiku wa leo (jana
usiku) 2 Julai, 2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,” Bunge
limeeleza.
Taarifa
ya Bunge iliyosambazwa na Kitengo chake cha Habari, Elimu na
Mawasiliano imebainisha kuwa chombo hicho kinaendelea kuratibu mazishi
kwa kushirikiana na familia ya marehemu na kuongeza, “taarifa
zitaendelea kutolewa.”
Profesa Maji Marefu ambaye alizaliwa 25 Mei, 1952, amekuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini tangu mwaka 2010.
No comments: