Rais Magufuli Kafanya Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Dkt. Ngenya Athuman Yusuf kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango
Tanzania (TBS).
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa
uteuzi wa Dkt. Ngenya Athuman Yusuf umeanza tarehe 30 Juni, 2018.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Ngenya Athuman Yusuf alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM).
No comments: