Rais Magufuli: Mikoa Ya Kusini Mngefanya Vurugu Kisa Koroshoi Ningetoa Kipigo Kizito
Rais
John Pombe Magufuli amesema alikuwa akisubiri wakulima wa mikoa ya
Lindi na Mtwara wafanye fujo kama jinsi ambavyo Wabunge wa mikoa hiyo
walivyokuwa wakidai na kueleza kwamba angewashughulikia kwa kipigo na
angeanza na jimbo linaloongozwa na Waziri Mkuu.
Rais
Magufuli ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akitoa hotuba yake baada
ya kuwaapisha Mawaziri na viongozi wengine ambao aliwateua siku ya jana
alipofanya mabadiliko madogo katika wizara yake.
"Watu
wanataka popularity, wengine nilisikia wanasema watachomewa nyumba,
nilimwambia Waziri Mkuu nataka nione wakifanya fujo. Ningewapa kipigo.
Tena ningeanza kwenye jimbo lake kama kuna shangazi zake ningeanza
kupiga hao. Nasema ukweli wala sifichi"
Rais
aliongeza "Lazima tufike mahali tuambizane ukweli, ndiyo maana
nilimwambia Katibu Mkuu CCM, aende Dodoma siku ya kupiga kura. Wabunge
wa CCM ambao hawakuwepo wachukuliwe hatua".
Katika
kuonyesha kukasirishwa na kitendo ambacho kilifanya na Wabunge wa Mikoa
hiyo ambo pia ni wa CCM, Rais Magufuli alisema anashangaa wanafanya
nini mpaka saizi kwenye Chama Cha Mapinduzi badala ya kuondoka.
"Watu
wanashangilia uongo, tumechoka, nilimuuliza Waziri Mkuu kuna wabunge
wangapi wa CCM, Mtwara na Lindi akasema wapo 17, nikasema bora waondoke
wote, hata Waziri Mkuu ni wa huko naye angeondoka, bado tungeweza
kuongoza nchi. Nilimpigia simu Katibu wa CCM tukae kwenye mpango huo.
Wangeondoka,"
Pamoja
na hayo, Rais Magufuli alisema "Siku ya kupitisha bajeti nikamwambia
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru nenda Bungeni ukaangalie wabunge
wangapi wa CCM hawapo bungeni uwalime barua, na kweli amewaandikia barua
wote. Japo wapo Wabunge waliokuwa na sababu za Msingi lakini kuna wale
ambao wamelimwa barua. Prof. Kabudi alikuwa amelazwa lakini kapokea
barua yake na ataambatanisha na vyeti vya hospitali"
Mbali
na hayo Rais amempongeza Naibu Waziri Mpya wa Kilimo na Umwagiliaji kwa
kuweza kupambana kuitetea serikali wakati wa hoja ya Korosho ilipokuwa
imepamba moto.
“Nakupongeza
Naibu Waziri wa Kilimo (Omary Mgumba) kwa kazi uliofanya Bungeni, huwa
nafuatilia michango ya CCM, mwingine anasema tukienda hivi tutashindwa,
kwa nini bado uko CCM, si utoke huko? Ulinyimwa nafasi ya kutetea hoja
yako, mmoja akapewa nafasi ya kukupiga na mwingine tena akakupiga, hiki
ulichokipata ndicho ulistahili, nakuomba ukashirikiane na wenzako Wizara
ya Kilimo." Alisema
No comments: