Familia ya Tundu Lissu kudai matibabu mahakamani
Wakati
mbunge Tundu Lissu akiendelea na matibabu nchini Ubelgiji, kaka yake,
Alute Mughwai amesema wanatarajia kwenda mahakamani kudai haki ya
kisheria ya matibabu ya mbunge huyo.
Akizungumza
jana Jumatatu Julai 2, 2018 na waandishi wa habari, Mughwai alisema
wanachukua hatua hiyo baada ya Bunge kuiandikia barua familia hiyo,
ikieeleza kuwa kuanzia sasa haitajishughulisha na matibabu ya mbunge
huyo.
Mughwai
alisema Juni 18, 2018 walipokea barua kutoka uongozi wa Bunge kuwa
haitajishughulisha na matibabu ya mbunge huyo kwa kuwa yuko nje ya nchi
kwa utaratibu binafsi.
“Limesema kwa kuwa anapatiwa matibabu uko nje ya nchi kwa utaratibu binafsi na hakufuata utaratibu wa matibabu,”alisema
Alisema
kutokana na hali hiyo wanaangalia utaratibu wa kwenda mahakamani
kuangalia kama mwakilishi huyo anahaki kisheria ya kupatiwa matibabu.
No comments: