Mbowe na Viongozi 8 wa CHADEMA wamemkataa Hakimu
Vigogo
tisa wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe
wamewasilisha ombi la kutaka Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,
Wilbard Mashauri kujitoa kusikiliza shauri lao.
Kufuatia ombi hilo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Julai 5, 2018 kutoa uamuzi katika kesi inayowakabili viongozi hao.
Uamuzi
huo wa mahakama umetolewa jana Jumatatu Julai 2, 2018 na Mashauri baada
ya washtakiwa hao kueleza sababu ya kutokuwa na imani nae.
“Baada
ya kusikiliza sababu za washtakiwa walizotoa hapa mahakamani za kumtaka
hakimu anayeendesha shauri hili kujitoa, Julai 5 mahakama hii itatoa
uamuzi kama hakimu huyo ajiondoe kuendesha shauri hilo au asijiondoe”
alisema hakimu Mashauri.
Wakili
wa utetezi, Peter Kibatala alisema wateja wake wamemueleza kuwa hawana
imani na hakimu Mashauri anayeendesha kesi hiyo na wanaomba ujitoe
kusikiliza shauri hilo, hivyo wanaomba nafasi ili waweze kueleza sababu
za kutokuwa na imani nae.
Aliyeanza kueleza sababu za kutokuwa na imani na hakimu huyo ni Mbowe ambaye alidai kuwa ana sababu kumi.
Baada
ya kupitia hoja za pande zote ambazo pia zilitolewa na washtakiwa
wengine, Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 5, 2018
atakapotoa uamuzi.
Washtakiwa
katika Kesi hiyo ni Mbowe, naibu makatibu wakuu, Salum Mwalimu
(Zanzibar) na John Mnyika (Bara); mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche;
mbunge wa Kawe, Halima Mdee; mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.
Wengine
ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vicent Mashinji; mbunge wa Iringa
Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.
Washtakiwa kwa pamoja wanakabiiwa na mashtaka 13.
No comments: