Serikali kuwaenzi Wanamichezo Wakongwe
Serikali
imeandaa mpango wa kuwaenzi watu mashughuri wakiemo wanamichezo
wakongwe ambao wamewahi kuliletea taifa heshima katika mashindano
mbalimbali akiwemo mwanariadha Mkongwe Bw. John Steven Akwhari.
Hayo
yamesemwa leo Mbulu Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe. Juliana Shonza alipomtembelea mwanariadha huyo nyumbani
kwake ambapo alipata fursa ya kuona medani , tuzo na vikombe alivyowahi
kushinda mwanariadha huyo.
“
Sisi kama Wizara tumeanzisha kampeni ya Uzalendo ambapo mwaka jana
tuliwaenzi wasanii wa zamani wa muziki na mwaka huu mnamo Oktoba 14 ni
zamu ya wanamichezo wakongwe akiwemo Bw. John Akwhari ” amesema Mhe.
Shonza
Alizidi
kueleza kuwa amevutiwa na jinsi mwanariadha huyo anavyotunza kumbukumbu
zake huku akiwataka wanamichezo na watu wengine kuiga mfano huo bora
ili kuviwezesha vizazi vijavyo kupata historia nzuri katika sekta ya
michezo.
Naye
Mwanariadha Mkongwe Bw. John Steven Akwhari amesema amefurahi kuona
Serikali inatambua na kuthamini mchango wake katika sekta ya michezo na
kuhaadi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kwa pamoja kuleta
maendeleo katika sekkta hiyo muhimu.
Bw.
John Akwhari ni mwanariadha wa zamani wa Tanzania wa kwanza kufungua
milango ya kushiriki riadha nje ya nchi ambapo alijizolea umaarufu
katika mashindano ya mwaka 1968 ya Olimpiki nchini Mexico ambapo licha
ya kuwa wa mwisho aliueleza umati kuwa nchi yake ilimtuma kumaliza mbio
na siyo kuanza mbio.
No comments: