Waziri Mkuu Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili Wa Mbunge Wa Korogwe Vijijini, Profesa Maji Marefu.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameongoza waombolezaji katika kuuaga mwili wa
aliyekuwa mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani maafufu
Profesa Maji Marefu.
Bw. Ngonyani ambaye alifariki dunia Julai 2, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi ameagwa leo (Jumatano, Julai 4, 2018) katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa wanafamilia, wabunge, wananchi
wa Korogwe pamoja na Watanzania kwa ujumla. Amewataka waendelee
kumuombea marehemu.
“Natoa
pole kwa wake wa marehemu, watoto na nawaomba tuendelee kuwa wavumilivu
na watulivu katika kipindi hiki. Tulimpenda sana lakini Mwenyezi Mungu
amempenda zaidi,”.
Kwa
upande wake, Katibu wa Bunge, Bw, Stephen Kagaigai akisoma wasifu wa
marehemu amesema Bw. Ngonyani alizaliwa Mei 25, 1956 katika wilaya ya
Songea mkoani Ruvuma.
Bw.
Kagaigai amesema marehemu alianza kuugua Juni 17 mwaka huu na Juni 18
alilazwa katika Hopitali ya Mkoa wa Dodoma na Juni 20 alihamishiwa
katika Hopitali ya Muhimbili.
Shughuli
hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi. Mkuu wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally, Spika wa Bunge, Bw. Job
Ndugai, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, Wabunge na wanafamilia.
No comments: