Wajapan Wameamua Kumuua Pweza Aliyetabiri Kuhusu mechi ya Japan Kombe la Dunia Huko Urusi
Pweza
anayeaminika kuwa na uwezo wa kipekee, na ambaye alikuwa amefanikiwa
kutabiri matokeo ya mechi zote za Japan katika Kombe la Dunia Urusi
ameuawa na kuuzwa sokoni awe kitoweo.
Pweza
huyo aliyekuwa amepewa jina la Rabio alikuwa amepata sifa si haba baada
ya kujaribiwa kwenye kidimbwi kidogo cha watoto na kuwa mtabiri stadi.
Aidha,
Kimio Abe, mvuvi aliyemvua kutoka baharini, amesema aliona ni heri
kumuuza ageuzwe kuwa chakula badala ya kuendelea kutabiri.
Amesema
kuwa alibaini angepata pesa nyingi iwapo angemuuza apikwe na kuwa
chakula kitamu cha Kijapani kwa jina sashimi kuliko kama angeendelea
kutumiwa kutabiri.
Hata
hivyo, Rabio ambaye alikuwa Pweza mkubwa alifanikiwa kubashiri matokeo
ya Japan dhidi ya Colombia na pia sare yao dhidi ya Senegal kwa kuhamia
maeneo mbalimbali kwenye kidimbwi chake.
No comments: