Mwanamke mbaroni wizi mtoto mchanga Mwanza
Mwanamke mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuiba mtoto wa kiume mwenye umri wa wiki tatu.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, alisema mwanamke huyo
aliyetambulika kwa jina la Paulina Mashiku (27) ni mkazi wa ukijiji cha
Mbugani wilayani Sengerema.
Alisema
mtuhumiwa huyo aliyekuwa ameolewa na mwanamume anayeishi maeneo ya
Bukoba visiwani anakojishughulisha na uvuvi kwa kipindi chote cha ndoa
yao hawajawahi kupata mtoto jambo lililosababisha mwanamke huyo
kumdanganya mumewe kuwa amepata ujauzito.
Juzi,
majira ya saa sita mchana alifanya kitendo hicho lakini siku mbili
kabla ya tukio, alipita katika kijiji cha Buliyaheke na kumwona mwanamke
akinyonyesha mtoto mchanga ndipo alipochukua jukumu la kumpigia simu
mumewe na kuwaaga majirani anakwenda hospitalini kujifungua.
Alisema
kesho yake alifika katika nyumba alipo mtoto huyo majira ya 4:00 usiku
na kumwona mama wa mtoto akiwa nje akipika wakati huo mtoto akiwa
amelala chumbani. Alipita mlango wa uwani na kumwiba mtoto huyo na
kurudi naye nyumba kwake huku akiwaeleza majirani kuwa amejifungua
salama.
"Jambo
hilo liliwapa wasiwasi majirani kwa kuwa walipata taarifa katika kijiji
cha Buliyaheke kuna mwanamke ameibiwa mtoto, hivyo wakatoa taarifa
kituo cha polisi.
“Baada
ya kupokea taarifa, polisi walifanya ufatiliaji wa haraka hadi eneo la
tukio kisha mtuhumiwa aliwekwa nguvuni na alipohojiwa alikiri ni kweli
alimwiba mtoto," alisema Msangi
Aliongeza
kuwa hali ya mtoto ni nzuri na tayari amekabidhiwa kwa mama yake mzazi
na polisi wako katika mahojiano na mtuhumiwa. Alisema pindi uchunguzi
ukikamilika atafikishwa mahakamani ili hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yake.
Kamanda
Msangi alitoa wito kwa wakazi wa Mwanza kuwa waangalifu na watoto wao
dhidi ya watu wenye nia ovu huku akiwataka waendelee kutoa ushirikiano
na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu mapema ili
wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
No comments: