England Yatika Robo Fainali Kombe La Dunia Ikiimaliza Colombia Kwa Penalyi 4-3
Timu
ya taifa ya England maarufu kama 'Simba watatu', imetinga hatua ya robo
fainali baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya penati 4-3 baada ya
dakika 120 kuisha kwa sare ya 1-1 dhidi ya Colombia kwenye mchezo wa 16
bora uliomalizika jana usiku .
England
ambayo iliongoza kwa bao 1-0 kutoka dakika ya 57 ilijikuta kwenye
wakati mgumu baada ya kusawazishiwa bao hilo katika dakika ya 90, hivyo
kulazimu mchezo kwenda katika dakika za nyongeza kabla ya penati kuamua.
Katika
mchezo huo mshambuliaji na nahodha wa England Harry Kane alifunga bao
la England hivyo kufikisha mabao 6 na kuifikia idadi sawa ya mabao kama
aliyofunga James Rodriguez wa Colombia kwenye fainali za mwaka 2014
nchini Brazil ambapo aliibuka mfungaji bora.
Jordan
Pickford amekuwa golikipa wa kwanza wa England kupangua penati kwenye
mechi ya mashindano tangu alipofanya hivyo kipa wa zamani wa England
David Seaman dhidi ya Argentina mwaka 1998.
Penati za England zimefungwa na Harry Kane, Marcus Rashford, Kieran Trippier na Eric Dier huku Jordan Henderson akikosa.
Kwa upande wa Colombia waliofunga ni Radamel Falcao, Juan Cuadrado na Luis Muriel huku Mateus Uribe na Carlos Bacca wakikosa.
No comments: