Rais Magufuli Kampa Ujumbe Mzito Balozi wa Marekani....." Wambie Boeing Wakamilishe Haraka Ndege Yetu ya Pili, Pesa Ipo"
Rais
wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtaka Balozi wa Marekani
afikishe salamu zake kwenye Kampuni ya ndege ya Boeing kuwa wakamilishe
haraka ndege ya pili inayotakiwa kufika Tanzania kwa kuwa hela za
kulipia zipo.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, wakati wa sherehe za kupokea ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyowasili leo kutokea Seattle nchini Marekani.
"Ndege
hizi ni matokeo ya Watanzania kulipa kodi na kuchapakazi. Nawapongeza
wote walioshiriki kikamilifu. Ndege zote hizi tumenunua kwa fedha zetu
wenyewe, hatujakopa kwa mtu. Tunataka Balozi wa Marekani utufikishie
salam Boeing kuwa ile Dreamliner ya pili waikamilishe haraka, hela
tunazo" - Rais Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli ameongeza kwamba "Madai kuwa Watanzania wengi
hawafaidiki na ndege hayana msingi. Wapo wengi wanaohitaji ndege bei
ilikuwa juu. Ndege hii imewafurahisha wengi na kama yupo mtu hajafurahia
tukio hili basi huyo atapata tabu sana!-Rais Magufuli
Pamoja
na hayo Rais amefafanua kuwa ndege hiyo imeletwa ili iweze kuimarisha
na kuongeza mapato ya utalii nchini kwa kuwa 70% ya watalii wanatumia
ndege.
Mh.
Rais amesisitiza kwamba "Ukiongeza ndege wasafiri wanaongezeka. ATCL
imeongeza wasafiri kutoka 4000 kwa mwezi mpaka 21,000 kwa mwezi.
Tunaboresha usafiri wa reli, majini na barabara. Waliodhani kuwa
maboresho ya Bandari hayana tija sasa wameaibika".

No comments: